Edufocus.co.ke

Quality Exams

Form 4 Kiswahili Paper 3 Isimu Jamii Questions from 2006 -2022

Published on May 7th 2024 | 5 mins , 819 words

2021 Machi 2022 

Mada: Sajili 

a.  Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. 

“Karibu, karibu! Keti. 

Naam, jitambulishe kwa jopo hili… Bwana Nuru, ni jambo lipi ambalo linakufanya kuamini kwamba nafasi hii inakuafiki wewe?” 

i.  Bainisha sajili ya makala haya.  Alama 1 

ii.  Eleza sifa nne za sajili hii kwa kurejelea makala haya.  Alama 4 

Wewe ni kinara wa chama cha Wanamawasiliano Bora shuleni mwako. Umepewa jukumu la kuwatangazia wenzako mashindano ya uogeleaji yakiendelea shuleni mwako. 

Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia. Alama 5 


 

 2020 : SAJILI

Umewahutubia wanaeneobunge lako kuwaomba wakuchague kuwa mbunge wao. Umegundua kwamba hujafanikiwa kuwavutia upande wako. 

Fafanua sifa kumi za lugha ungetumia kuwavutia. 


2019

Wewe ni muhubiri katika Maabadi ya Shamu. Umealikwa kuwahubiria wanafunzi wa shule ya Upili ya Lulu.

 Fafanua sifa kumi za lugha utakayotumia.


2018
Ndugu wapenzi, waumini wenzangu, mbazi hii haionyeshi huruma ya Mwenyezi Mungu kwetu wakosefu tu bali pia inatufunza umuhimu wa unyenyekevu na msamaha. 

a.  Bainisha sifa tatu za sajili ya kidini zinazojitokeza katika makala haya. al. 3 

b.  Fafanua vipengele vingine saba vya kimtindo ambavyo mhubiri huyu angetumia kufanikisha mazungumzo yake. al. 7


2017

 Ndugu wapenzi, waumini wenzangu, mbazi hii haionyeshi huruma ya Mwenyezi Mungu kwetu wakosefu tu bali pia inatufunza umuhimu wa unyenyekevu na msamaha. 

a.     Bainisha sifa tatu za sajili ya kidini zinazojitokeza katika makala haya. al. 3 

Fafanua vipengele vingine saba vya kimtindo ambavyo mhubiri huyu angetumia kufanikisha mazungumzo yake. al. 7 

2017

 

“Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, mahakama hii imethibitisha bila chembe ya shaka kwamba wewe mshtakiwa, Bi. 

Mlachake Chauchau ndiye uliyepika pombe haramu ambayo ilisababisha vifo vya raia hamsini na kupofuka kwa wengine mia 

moja. Unahukumiwa kwa kosa la mauaji.” 

a.     Bainisha sajili ya makala haya kwa kutoa mifano miwili kutoka kwenye makala. al 2 

Fafanua sifa nyingine nane za sajili hii ambazo zingejitokeza katika makala haya. al 8 

2016

 Kwa kutolea mifano maridhawa, eleza kaida zozote tano ambazo matumizi ya lugha hutegemea katika jamii.


2015

 

Mtu I: wewe njoo hapa! (kwa sauti kubwa). Fanya upesi! 

Mtu II: (Anakimbia mbio) Naja sir. 

Mtu I: (Anamtazama) Unajifanya mwerevu? Mtu II: Hapana sir…eh…afande.

Mtu I: Jina? 

Mtu II: Samwel Kibao. 

Mtu I: (Huku anaandika) Lete kitambulisho. Mtu II: Sina hapa sir. 

Mtu I: Huna kitambulisho? Utafanyiwa booking vipi? 

Mtu II: Naomba… 

Mtu I: Naomba! Nomba! Unaomba nini? Wazururaji kama nyinyi tunawajua. 

Mnajidai hamjui kuna curfew. Mnajiponza wenyewe na kuwahasiri wenzenu. Kisha, “serikali saidia”. Usiniharibie muda wangu.(akiashiria). Ingia ndani! Utakuwa mgeni wetu leo. Tutakukirimu chakula na chumba. (anamsukuma ndani) 

a. Bainisha sajili ya makala haya. al 2 

b. Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea makala haya. al 8 


2014

 Umepewa jukumu la kuwazungumzia vijana wenzako kuhusu umuhimu wa uwekezaji. Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia. 


 2013

Haya ngar’a ng’ara leo! Nguo motomoto. Ng’ara leo kwa bei rahisi. Hamsini hamsini shati. Kuona ni bure. Bure kwa bure. Shika mwenyewe ujionee. Bei nafuu. Bei ya starehe. Haya haya. usikose mwanangu! 

Hamsa! Fifty! Hamsa! Fifty! Hamsa na nyingine. 

 

a. Bainisha sajili ya mazungumzo haya. al 2 

b. Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea kifungu hiki. al. 8 


2012


 

Elezakwaufupijinsimamboyafuatayo yanavyodhibitimifeidoyalugha. 

(a)   Mazingira      (alama 4) 

(b)  Madhumuni   (alama 2) 

(c)  Malezi       (alama 4) 


 2011

(a)  Bainisha changamoto tano zinazoikabili lugha ya Kiswahili kama somo katika shule za upili nchini Kenya. (alama 5) 

(b)  Eleza namna tano za kukabiliana na changamoto ulizobainisba hapo juu. (alama 5) 



 2010

"Benki yenyewe haina kitu ... CD4 count yake iko chini ... Ni emergency ... 

Tutampoteza ikikosekana." 

 (a)  Taja sajili inayorejelewa na manerio haya. (alama 2) 

 (b)   Fafanua sifa nne zinazohusishwa na sajili hiyo (alama 8) 

2009

 Eleza majukumu matano matano matano ya Kiswahili kama lugha ya Kitaifa na Kimataifa. 

2008

 Eleza huku ukitoa mifano sifa tano za kimsingi zinaaotambulisha sajili ya mazungumzo   (alama 10) 

2007

Huku ukitoa mifano mwataka, fafanua kaida tano kaiika jamii ambazo matumizi ya lugha hutegemea. 


2006

 

Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheria za nchi, umepatikana na hatia ya kutatiza utulivu wa raia wapenda amani kwa kuwatusi na kutisha kuwapiga. 

Kiongozi wa mashtaka amethibitisha haya wa kuwaleta mashahidi ambao wametoa ushahidi usiotetereka kuhusu vitendo vyako katika tukio hilo. Korti hii imeonelea una hatia na imeamuru ufungwe jela kwa muda wa miaka miwili bila faini ili liwe funzo kwako na kwa wenzako wenye tabia kama zako. Una majuma mawili kukata rufani. 

a)  Lugha iliyo katika kifungu hiki hutumika katika muktadha upi?(alama 1) 

b)  Toa ushaidi wa jibu lako(alama 3) 

Zaidi ya sifa zilizo katika kifungu hiki, eleza sifa zingine sita za matumizi ya ligha katika muktadha huu.(alama 6) 

Download File